Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari 200 ya mchanga yapata vibali

62055 Pic+magari

Tue, 11 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi amesema jumla ya magari 200 yenye ujazo tofauti yamepewa vibali vya kubebeba mchanga visiwani hapa baada ya kukidhi vigezo.

Dk Ussi amesema magari hayo ni miongoni mwa 774 ambayo wamiliki wame walituma maombi ya kufanya kazi hiyo wizarani hapo mwaka huu. Alisema kati ya maombi hayo 654 yalitoka Unguja na 120 Pemba.

Akizungumza leo Jumatatu June 10, 2019 katika mkutano wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Unguja wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Konde, Omar Seif Abeid, amesema wizara ilifanya upembuzi wa maombi hayo kiwilaya ili kutoa fursa sawa ya kupatikana huduma hiyo, ambapo miongoni mwa vigezo muhimu vilivyozigantiwa ni ujazo wa gari (tani).

Katika swali lake, Abeid aliuliza, “licha ya kuwepo utaratibu maalumu wa kusajiliwa gari za kubeba mchanga. Je, katika maombi hayo wadau walishirikishwa ili kuona usawa unafanyika kwa kila mwenye vigezo kupatiwa haki yake ya msingi? Vibali hivyo vimetolewa kwa kipindi cha miezi mitatu kwa thamani ya Sh25,000.

Chanzo: mwananchi.co.tz