KAMPUNI ya Magare inayohusika na uhandisi wa umeme na mitambo ya viwandani pamoja na migodini imetoa msaada wa mashine ya Photocopy,Printer na kompyuta moja katika shule ya sekondari ya Isagehe iliyopo katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano wa vitu hivyo,Mkurugenzi wa kampuni ya Magare,Mabula Magangila alisema wametoa vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa Elimu bora ikiwemo pamoja na utoaji wa mitihani na nukuu mbali mbali za shule.
Magangila alisema kampuni yao iliahidi wakati wa mahafali ya kidato cha nne,Oktoba 22 mwaka huu kuwa ingeleta printa,mashine yaphotocophy na Kompyuta na wamefanikisha kutimiza ahadi hiyo.
‘’Tunahitaji wahitimu walio bora na Magare company limited tumejitoa kwajili ya kufadhili shule hii ili iweze kuwa bora zaidi. Kiukweli kampuni yetu imeguswa sana na kuamua kuchangia shule hii’’ Magare alisema.
Alisema anawaomba walimu na wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha hakuna division 0. Alisema walimu washirikiane kuweza kutafta matokeo mazuri na bora zaidi.
Alisema kampuni ya Magare iliahidi kuweka mtandao wa maji katika shule hiyo na tulifanikisha kuweka maji shule hapo kwa asilimia 100.
Magangila alisema katika ahadi yao nyingine waliahidi kuajiri walimu sita wa masomo ya sayansi na biashara na tayari walimu wameshajiliwa na wataanza kazi rasmi Januari wakati shule hiyo itakapokuwa imefunguliwa.
Mkuu wa shule ya Isagehe,Makoye Nyanda alisema anaishukuru sana kampuni ya Magare kwa msaada wao na alisema anaiomba kampuni hiyo iendelee kuwasaidia mara kwa mara.
Alisema anawaomba wadau wengine waige mfano wa kampuni ya Magare na kuweza kuwasaidia shule hapo. Diwani wa kata ya Kagongwa wilayani Kahama,Ismail Masolwa alisema anaishukuru kampuni ya Magare kwa kusaidia shule hiyo.
Mwanafunzi kutoka shule ya Isagehe,Nsia Jeta alisema anashukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na alisema watasoma kwa bidii sana kuweza kufaulu kwa bidii.