Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta ya bure yazua balaa Tabora

Mafutapiic Nsm Mafuta ya bure yazua balaa Tabora

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madereva bodaboda na bajaji zaidi ya 500 wa manispaa ya Tabora leo Jumapili Januari 22, 2023 wamegombea mafuta yaliyotolewa bure na mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka.

Kutokana na vurugu zilizotokea katika kituo vituo viwili vya mafuta, imelazimika utaratibu wa kutoa mafuta kusitishwa kwa muda ili kupata fursa ya kujipanga vizuri.

Awali walikuwa wameandikishwa majina yao na baada ya mbunge huyo kuzungumza nao, aliwaeleza wakaweke mafuta kwenye vituo viwili lita tatu kila mmoja.

Mwakasaka amesema wanapaswa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika miradi ya maendeleo inayojengwa sehemu mbalimbali nchini ikiwemo ya manispaa ya Tabora.

"Nawaomba sana tusiwasikilize wale wanaobeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa SGR, amewataka vijana kuheshimu taratibu zilizowekwa na nchi katika miradi ya maendeleo ambapo mhusika anapewa fursa ya kuweka watu anaowataka katika kutekeleza mradi aliopewa.

"Kumekuwa na malalamiko kuhusu ajira ujenzi wa reli ya kisasa kwa vijana kuwa wanaopata kazi ni wanaotoka nje ya mkoa wa Tabora na wenyeji kutopewa fursa ya ajira. Wapo wenyeji baadhi waliopata ajira ikiwemo ya udereva ambao wanaendelea kufanya kazi katika kampuni ya Yepi Markenzi inayotekeleza ujenzi wa mradi huo kutoka Makutupora hadi Tabora," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live