Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuruko yasomba nyumba 109 Dodoma, mamia wakosa mahali pa kuishi

Mafuruko yasomba nyumba 109 Dodoma, mamia wakosa mahali pa kuishi

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Nyumba 109 katika  kijiji cha Igandu Stesheni Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma zimesombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Februari 6, 2020 mwenyekiti wa kijiji hicho,  George Yona amesema nyumba zimesombwa na maji kuanzia Februari 2, 2020 hadi usiku wa kuamkia leo.

Yona amesema mbali na wananchi hao kukosa makazi,  hawana chakula.

“Wakazi wa nyumba 109 hawana makazi wanaishi kwa majirani walionusurika katika mafuriko hayo, wapo wengine hawana hata sehemu ya kujihifadhi, tunaomba Serikali itusaidie,” amesema Yona.

Amebainisha kuwa walitoa taarifa kwa uongozi wa kata ya Igandu pamoja na tarafa lakini hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa.

Gipson Makonde, mkazi wa kijiji hicho amesema familia yake ya watu wanane haina pa kuishi baada ya nyumba kubomoka.

Pia Soma

Advertisement
Naye Yaledi Job amesema katika familia yao wapo wanne na wote hawana mahala pa kuishi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz