Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yawakosesha makazi watu 90 mkoani Manyara

94693 Manyara+ic Mafuriko yawakosesha makazi watu 90 mkoani Manyara

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hanang'. Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimesababisha Ziwa Bassotu wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara kujaa na maji kwenda katika makazi ya watu.

Amesema hali hiyo imesababisha wakazi 90 wa Wilaya hiyo kukosa makazi.

Mbali na kukosa makazi, mawasiliano ya Wilaya ya Hanang' na Mbulu yamekatika baada ya barabara ya Katesh-Haydom kutopitika.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Jackson John amesema  kwa sasa wanaishi kwa ndugu na jamaa na majirani.

"Hizi mvua zinazoendelea kunyesha ni kubwa zaidi ya zilizonyesha hivi karibuni kwa sababu zimesababisha  madhara makubwa kwetu tunaoishi karibu na ziwa," amesema.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Paul Kasabago amesema aliagiza barabara ya Katesh-Haydom isitumike kwa lengo la kuepusha madhara.

Pia Soma

Advertisement

Amesema hivi sasa barabara hiyo ni hatari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kusababisha madaraka kukatika.

"Nimewaagiza askari wa kituo cha polisi Bassotu kuzuia matumizi ya barabara hiyo hadi wataalamu watakaporuhusu ili kuepusha ajali zisizo na lazima," amesema Kasabago.

Diwani wa Bassotu,  Samuel Qawoga amesema hivi sasa wananchi hao 90 wanasaidia vyakula na majirani.

Chanzo: mwananchi.co.tz