Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yawaacha bila makazi wananchi 4,500 mkoani Lindi

93259 Pic+mvua Mafuriko yawaacha bila makazi wananchi 4,500 mkoani Lindi

Tue, 28 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kilwa. Zaidi ya wananchi 4500 wa vijiji sita wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 27, 2020 mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Kilanjelanje, Nanjirinji A Ruatwe, Njinjo, Nakiu na Nanjirinji B.

Amesema mbali na nyumba kubomoka, mashamba na mifugo ya wananchi hao nayo imesombwa na maji.

“Mafuriko yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo,” amesema Ngubiagai.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema  timu ya uokoaji imekwenda eneo lililokumbwa na mafuriko kwa boti  kunusuru maisha ya wananchi, kwamba wananchi hao watapelekwa katika maeneo yaliyotengwa.

Amewataka watu wa kada mbalimbali kutoa msaada kwa wananchi hao.

Pia Soma

Advertisement
“Tunaendelea kuwaokoa na kuwapeleka maeneo ambayo tumeyatenga. Tunahitaji msaada wa chakula, dawa, nguo na vitu vingine muhimu,” amesema Ngubiagai.

Chanzo: mwananchi.co.tz