Korogwe. Watu saba wamefariki dunia na kaya zaidi ya 300 Wilayani Korogwe hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na zingine kujaa maji kutokana na mvua inayoendelea kunyesha wilayani humo.
Akizungumza na Mwananchi usiku huu, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Edward Bukombe amesema vifo hivyo vimetokea katika vijiji vya Bungu, Dindira na Vingo, wilayani Korogwe.
Akizungumzia hali hiyo mapema mchana wa leo Jumatano Oktoba 9,2019, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa alisema mafuriko hayo yameathiri maeneo ya
Majimbo ya Korogwe Mji na Korogwe Vijijini.
Ameyataja maeneo yaliyoathirika ni Masuguru, Chuo cha Ualimu cha Early Education kilichopo Mbeza, Soko la Manundu, Kilole na Mgombezi.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mji, Mary Chatanda amesema kwa kushirikiana na viongozi wengine, wamelazimika kufanya kazi ya kuwakoa watu ambao nyumba zao zimezingirwa na maji ya Mto Pangani na Mto Mbeza.
Pia Soma
- Wake wa Rooney, Vardy wapeana vidonge Instagram
- Benki ya DCB yazindua akiba ya mpango wa elimu
- Mkuu wa mkoa Mnyeti afunga migodi ya madini ya ujenzi
“Tupo katika harakati za kuwahamisha wananchi, hali ni mbaya sana
Nyumba za kuishi, majengo ya shule na ya taasisi nazo zimejaa maji ila kwa sasa tunawaokoa watu kwanza,” amesema Chatanda.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Gwakisa alisema idadi kamili ya waliokosa
mahala pa kuishi pamoja na madhara yaliyotokana na mafuriko hayo
yatatolewa baada ya kamati ya ulinzi na usalama pamoja nay a maafa
kukaa na kufanya tathimini.
“Bado tunakusanya taarifa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilayani hapa
halafu tutakutana kamati za ulizni nay a maafa kufanya tathmini ya
madhara yaloiyotokea”alisema Gwakisa.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Tanga, Alfread Ndumbaro amewataka madereva kutotumia barabara za Old Korogwe, Magoma Songea
Kilole na Kwasunga kwa kuwa madaraja yake yameathirika.
“Madereva na wananchi wasubiri kwanza mafuriko yapungue ili kusitokee
madhara kwa kuwa madaraja ya Mto Msangazi pale ilipotokea ajali ya No
Challenge miaka ya nyuma na kuua watu wengi,maji yanapita juu na njia
Haionekani na Magoma daraja limemegwa upande,” amesema Ndumbaro.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Tanroads imesambazwa katika maeneo hatarishi kwa ajili ya kutoa msaada.