Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yaua 28 Morogoro, watano pwani

Mafuriko2285 Mafuriko yaua 28 Morogoro, watano pwani

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji Mkuu wa Serikali, amesema tathmini iliyofanyika ya athari ya mvua katika mikoa ya Morogoro na Pwani imebaini kuwa watu 28 wamefariki dunia mkoani Morogoro na wengiine watano mkoani Pwani.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameeleza hayo leo Aprili 12,2024 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu athari za hali ya mvua na mafuriko yanayoendelea nchini.

Amesema mkoani Morogoro mpaka sasa maafa hayo yamesababisha vifo vya watu 28 katika halmashauri nane za mkoa huo na kubomoa nyumba 1,035 na nyingine 6,874 zimezingirwa na maji.

“Kuna vifo vya watu watano, viwili katika wilaya ya Rufiji na viwili Kibiti na Kisarawe kifo kimoja, majeruhi wawili wilayani Kibiti na majeruhi watatu Kisarawe, lakini kuna uharibifu wa mazao mengi ya chaklula mahindi, mpunga, ufuta, ndizi mihogo na mtama.

“Makazi ya barabara, makazi, madaraja nguzo ya umeme, shule na kituo cha afya mhoro Rufiji kimesomwa na maji,” amesema. Ameeleza kata 12 kati ya 13 ya wilaya ya Rufiji na kata tano kati ya 13 za wilaya ya Kibiti na kata moja ya Kisarawe zimeathiri na watu 1,014 wameokolewa katika wilaya ya Rufiji pekee.

Pia hekari 34,970 za mazao zimeathirika pamoja na mifugo inayofikia 1,466 na miundombinu mbalimbali kuanzia reli ya Tazara, barabara, makalavati, barabara katika halamshauri hizi nane zimeathiri vibaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live