Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yatikisa Kongwa, DC afunguka

Mafuriko Md Mafuriko yatikisa Kongwa, DC afunguka.

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko ya maji  mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara, yamesababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma, baada ya kufunga eneo la Kongwa mkoani Dodoma kwa saa kadhaa. 

Akizungumza nasi kwa njia ya simu, jana tarehe 9 Januari 2024, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeka Simon Mayeka amesema mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika barabara eneo la Kongwa, na kusababisha magari na raia kushindwa kuitumia.

Mayeka amesema kwa sasa maji hayo yamepungua na kwamba magari yameanza kuruhusiwa kutembea kwa awamu, huku akitaja athari za mafuriko hayo kuwa ni gari moja lililolazimisha kupita kabla ya kuruhusiwa na kudondoka. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa au kupoteza maisha kufuatia mafuriko hayo.

“Ni sahihi kulikuwa na hali mbaya ya mafuriko toka asubuhi lakini sasa maji yameshapungua na tumeanza kuruhusu magari machache yapite kwa awamu. Athari kwa maana ya binadamu kupoteza maisha hakuna ila kuna gari lilijaribu kupita kabla ya askari kuruhusu lilidondoka,” amesema Mayeka na kuongeza:

“Chanzo cha mafuriko haya ni maji tunayopokea kutoka wilayani Kiteto ambako kunanyesha mvua sababu sisi huku mvua haikunyesha na sababu Kongwa iko chini maji yanajaa.”

Kuibuka wa taarifa hizi kumekuja baada ya baadhi ya wananchi kusambaza video zinazoonyesha barabara hiyo kujaa maji huku magari yakiwa kwenye mlolongo wa foleni baada ya kukwama kupita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live