Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko: Wananchi 500 wakosa makazi Babati

Makazi Babati 0c50d49 Wananchi 500 wakosa makazi Babati

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani wakazi zaidi ya 500 wa Babati Vijini, hawana pa kuishi wala chakula kutokana na Mashamba yao kusombwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendela kunyesha katika maeneo mbalimbali na kusababishwa kujaa kwa Ziwa Manyara.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini, na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Daniel Sillo, amewatembelea na kuwapa pole waathiriwa na Mafuriko hayo.

Sillo pia amekabidhi magunia 10 ya mahindi huku akiwataka wananchi hao kuwa watulivu na kusaidiana, wakati Serikali ikiendela na utaratibu mwingine wa kuchukua hatua za usaidizi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbogo amewaagiza wataalamu kuendelea kufanya tathmini ya maafa hayo na pia kumuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri kuhakikisha wanatoa tahadhari kwa Wananchi kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Diwani wa Kata ya Magara, Jocob Elias amesema Wananchi wamekuMbwa na adha hiyo tangu Januari 2024 kwa sababu maji hayo yanatoka katika mito inayotoka Babati, Ziwa Burunge na Ziwa Manyara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live