Zaidi ya watu elfu nne Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamekosa makazi kutokana na mafuriko ambayo yametokea kuanzia mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu yaliyosababisha nyumba zao zaidi ya mia tisa kujaa maji na nyingine kusombwa na maji.
Zaidi ya watu elfu nne Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamekosa makazi kutokana na mafuriko ambayo yametokea kuanzia mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu yaliyosababisha nyumba zao zaidi ya mia tisa kujaa maji na nyingine kusombwa na maji. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameyasema hayo wakati akitoa tathmini ya madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo na kuwaomba wadau wa maendeleo kujitokeza kutoa msaada kwa waadhiriwa wa mafuriko hayo.