Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko Kilosa kaya zaidi ya 120 zakosa makazi

Shaka Kilosa Mafuriko (600 X 278) Mafuriko Kilosa kaya zaidi ya 120 zakosa makazi

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amelazimika kutembea zaidi ya KM 5 ndani ya maji ili kujinusuru baada ya yeye na Timu yake kuzingirwa na maji wakati akikagua shughuli za uokoaji wa Wananchi waliopata mafuriko kufuatia kujaa mji kwa Mto Miombo baada kupokea maji mengi kutoka milimani na kupelekea kaya zaidi ya 120 kuathirika.

Awali DC Shaka na Wajumbe wa Kamati ya Usalama walifika eneo ambalo daraja linalounganisha Vijiji vitatu katika Kata ya Nyameni Zombo limesombwa na maji na kusababisha huduma za usafiri na usafirishaji kusimama lakini wakati wakitoka katika eneo hilo wakajikuta wamezungukwa na maji na kulazimika kuanza kutembea kujinusuru sambamba na kuwasaidia Wananchi wengine ambao bado walikuwa katika makaazi yao.

Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha milimani na hakuna athari za kibinadamu zilizoripotiwa zaidi ya kuharibu miundombinu ya madaraja, barabara na makazi ya Wananchi ambapo zaidi ya kaya 120 zimeingiliwa na maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live