Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga amewapa mbinu mafundi sanifu na wahandisi nchini itakayosaidia kushindana na wenzao kwenye soko ajira la Jumuiya Afrika Mashiriki (EAC).
Mwakalinga amesema mbinu hiyo ni pamoja kujijenga uwezo na kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia fursa zilizopo za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, jambo alilodai kitakuwa dawa na kinga kwa Watanzania.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 24, 2019 katika kongamano la pili la mwaka la mafundi sanifu lililoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa kuna presha inakuja kwamba EAC ikiwa kitu kimoja kutakuwa na changamoto ya ajira, wote watashindanishwa.
“Mchakato wa kufikia hatua hiyo bado haujasainiwa. Tunamshukuru Rais John Magufuli maana tungejikuta tuna wageni hapa nchini, "amesema Mwakalinga.
Ametumia fursa hiyo kuhimiza upendo kati ya mafundi sanifu na wahandisi akitaka wapendane badala ya kubaguana kwamba kila mmoja anamtegemea mwenzake katika utekelezaji wa majukumu.
Pia Soma
- Vifo vya watoto vinavyotikisa dunia
- Mvutano wa Tanesco, makandarasi wamuibua naibu waziri
- Mganga wa jadi adakwa kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano, alitishia kumgeuza msukule
- Hawa ndio mabalozi wa utalii Tanzania, Mbwana Samatta, Diamond na Ali Kiba ndani
Mwenyekiti wa bodi ya ERB, Profesa Ninatubu Lema alimweleza Mwakalinga kuwa bado kuna changamoto ya uhaba ya mafundi sanifu na tangu waanze kusajiliwa mwaka 2014 wamefikia 112.