Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maeneo yaliyopigwa na Kimbunga Hidaya kupewa kipaumbele

Hidaya Hidayaaa Mafurikooo .png Maeneo yaliyopigwa na Kimbunga Hidaya kupewa kipaumbele

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maeneo manane kupewa msukumo athari za Kimbunga Hidaya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kila mamlaka iweke kipaumbele cha kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa maafa nchini.

Amesema athari za Kimbunga Hidaya zinahitaji hatua za haraka na ushiriki wa wadau wote katika mfumo wa usimamizi wa maafa.

Hayo ameyasema leo Alhamisi Mei 9, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati wa maswali ya papo kwa papo

“Kama tulivyosikia na kushuhudia kupitia vyombo vya habari, athari za Kimbunga Hidaya zinahitaji hatua za haraka na ushiriki wa wadau wote katika mfumo wa usimamizi wa maafa. Hivyo naomba sasa niweke msisitizo kuhusu masuala yafuatayo:

“Katika maelezo niliyoyatoa siku ya Alhamisi Aprili 25, 2024 wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo hapa bungeni, nilisisitiza kuwa kamati za maafa za wilaya na mikoa ziendelee kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa tahadhari kwa wananchi na kuwasaidia kwa wakati pindi maafa yanapojitokeza.

Leo nasisitiza tena kuwa, sambamba na kamati hizo, wizara zote za kisekta zinazohusika na usimamizi wa maafa ziendelee kushirikiana na kamati hizo za ngazi ya mikoa na wilaya ili kuharakisha suala la kurejesha hali.”

Akitoa taarifa hiyo kuhusu Kimbunga Hidaya Majaliwa ametoa pia maelekezo kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wanapopata taarifa za uwepo wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ikiwemo vimbunga na dhoruba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live