Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maeneo ya Ziwa Victoria kinara wa bandari bubu Tanzania

87829 Bandari+pic Maeneo ya Ziwa Victoria kinara wa bandari bubu Tanzania

Fri, 13 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja, bandari bubu 164 katika maeneo ya maziwa na bahari nchini Tanzania, huku maeneo ya Ziwa Victoria yakitajwa kuwa kinara wa utitiri wa bandari hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA, Deusdedith Kakoko amesema upo mkakati wa kuhakikisha bandari zote ambazo ni bubu zinarasimishwa na kusimamiwa na mamlaka hiyo.

Kakoko anasema mpango huo utahusu bandari zote ambazo awali zilikuwa hasimamiwi na mamlaka hiyo zikiwamo za watu binafsi kwa ajili ya biashara, taasisi kwa ajili ya shughuli za kijamii na za familia hata kama inahudumia mtumbwi mmoja.

“Tunataka kuzifanya bandari bubu zote kuwa rasmi, hii itatusaidia kudhibiti uingizaji wa silaha haramu, dawa za kulevya na kuhakikisha Serikali inapata mapato stahiki. Mpaka Desemba, 2018, bandari bubu zilikuwa 437, lakini baada ya kuanza udhibiti zimekuwa zikiibuka mpya na sasa zipo 601,” amesema Kakoko.

Amesema endapo itaonekana kuwa kila wanapodhibiti zinafunguliwa mpya, basi zitakazokuwa zinafunguliwa zitakuwa zinafungiwa na kama hiyo haitoshi, vyombo vingine vya dola vitatumia mamlaka yake kudhibiti jambo hilo ambalo lazima liishe.

Kakoko ameongeza kuwa bandari hizo zitapangwa kwa viwango sita na zitakuwa kisheria na kuwekwa katika kanuni.

Zitasimamiwa kulingana na ukubwa wa biashara katika bandari hiyo na bei zitakuwa rafiki kwa watumiaji kama ilivyokuwa awali, inaweza ikapungua au kuongezeka kidogo.

“Tayari tumefanya mazungumzo, wale waliokuwa wanasimamia bandari hizo ili kuwa na ushirika mzuri tutakapoona inabidi, tutaboresha bandari hizo ili ziwe na hadhi inayokubalika, lakini baada ya hapo mapato yatakayopatikana tutapata na sisi (TPA) hata kama ni senti moja, lakini kuna maeneo ambayo hatutatoza mwanzoni,” amesema.

Amesema TPA itaingia mkataba na wasimamizi wa zamani wa bandari hizo wa zamani, waweze kushirikiana katika uendeshaji lakini pia wataweka mifumo ya Tehama ili kuweza kujua mapato yanayopatikana, kiwango cha mzigo na aina ya mizigo inayopita katika bandari hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz