Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya watu Mwanza wamuaga Magufuli

MWANZA WEB Maelfu ya watu Mwanza wamuaga Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: eatv.tv

Maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na wa maeneo jirani wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini humo.

Submitted by Agnes Kibona on Jumatano , 24th Mar , 2021 Wananchi wa Mwanza waliojitokeza kumuaga Hayati Dkt. John Magufuli

Akizungumza awali kabla ya kuanza kuaga kwa wakazi wa Jiji hilo, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, aliwapa salamu wana Kanda ya Ziwa zilizotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye amewataka kuendelea kushikamana na kuwa na upendo kama awali.

"Mheshimiwa Rais anawasihi katika kipindi hiki cha huzuni anawaomba sana kwanza muwe watulivu, tuendelee kufanya shughuli hizi tukiwa bado na huzuni tukisubiri siku ya kumfikisha kwenye nyumba yake ya milele Dkt. Magufuli, anatuomba tuendelee kushikamana, kushirikiana, kupendana kama tulivyokuwa huko awali," amesema Mhe. Majaliwa. 

Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, leo Machi 24 umeagwa Mwanza na unasafirishwa mpaka Chato kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wakazi wa Chato na familia kumuaga hapo kesho Machi 25 na Machi 26 atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kijijini kwake Chato.

Chanzo: eatv.tv