Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani watakiwa kusimamia ujenzi wa madarasa

6762f3b19295cde2c79ac61406e38858 Madiwani watakiwa kusimamia ujenzi wa madarasa

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amewataka madiwani wa jiji la Tanga kusimamia ujenzi wa madarasa kwenye maeneo yao na yakamilike kwa wakati.

Maagizo hayo aliyatoa wakati wa hafla ya kuwaapisha madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo ambalo aliwataka wahakikishe wanasimamia ujenzi wa vyumba hivyo ili ukamilike na wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze masomo kwa wakati.

Alisema kuwa kila diwani akaangalie kwenye kata yake kama shule zina madarasa ya kutosha na madawati na kama kuna uhaba wajue ni juhudi gani za kuchukua ikiwemo kuwashirikisha wananchi ili kumaliza uhaba huo.

"Nendeni mkahamasishe wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili serikali itakapokuja kuchangia ikute kuna juhudi tayari zimeshachukuliwa kwani hili la upungufu linatuhusu sote," alisema RC Shigela.

Naye, mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ummy Mwalimu wana upungufu wa vyumba vya madarasa 44, kwa ajili ya wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza.

"Muda hautoshi wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wanatakiwa kuanza shule Januari 8, mwakani, hivyo niwaombe madiwani wenzangu tukahakikishe madarasa yanaisha kwa wakati," alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji alisema kuwa tayari wameshaanza jitihada za kujenga vyumba hivyo katika baadhi ya shule zenye uhitaji mkubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz