Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wamtimua kazi mtumishi, wawili wapewa onyo

Madiwanipic Baraza la Madiwani halamashauri ya wilaya ya Same

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro limemfukuza kazi mtumishi wa idara ya afya katika hospitali ya wilaya ya Same na kutoa onyo kali kwa wengine wawili na kuwakata asilimia 15 ya mishahara yao kila mmoja kwa muda wa miaka mitatu.

Hayo yamejiri Alhamisi Septemba 2, 2021 katika kikao cha baraza la madiwani.

Akisoma uamuzi ya kamati ya nidhamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Same, Yusto Mapende amesema Wilfred Mushi amefukuzwa kazi na kwamba amekuwa na matukio ya kujirudia ya ulevi uliokithiri, lugha ya matusi kwa watumishi wenzake na wagonjwa.

Mapande amewataja waliopewa onyo kali kuwa ni muuguzi msaidizi wa zahanati ya mkonge kata ya Kihurio, Ally Saidi Ally ambaye anakabiliwa na makosa ya utoro kazini na kutumia lugha chafu kwa wagonjwa wakati wa kutoa huduma.

Mtumishi mwingine ni Hatibu Mgonja ofisa mtendaji wa kata ambaye anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za Serikali hivyo kupewa onyo kali sambamba na kukatwa mishahara.

"Kama baraza tumeazimia kwa pamoja kumfukuza kazi mtumishi huyu ambaye amekuwa msumbufu mno ameonywa mara nyingi lakini tumeona sikio la kufa halisikii dawa hivyo tumeazimia kwapamoja afukuzwe apishe wengine wenye utayari wa kufanya kazi kwa ufanisi."

"Pia hawa wawili tumeamua kuwapa onyo kali ili kama wameelewa walichokosea wabadilike vinginevyo hatutavumilia mtumishi ambaye anaweza kuleta athari katika jamii lakini pia hawa tutawakata asilimia 15 ya mishahara yao kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, amesema Mapande.

Chanzo: Mwananchi