Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wambana DED Dar

33273 PIC+MADIWANI Tanzania Web Photo

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wamemtaka Mkurugenzi wa jiji hilo, Spora Liana kuwaunganisha wajasiriamali na masoko.

Madiwani hao walitoa rai hiyo walipotembelea eneo lililotengwa na Halmashauri ya jiji kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo lililopo Mwananyamala.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 24, 2018 Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo amesema wajasiriamali wamepata eneo la kufanyia shughuli zao, watakapozalisha bidhaa nyingi kutakuwa na changamoto ya masomo.

Amesema kwa kulitambua hilo Mkurugenzi wa jiji awaunganishe na masomo kulingana na bidhaa wanazozalisha.

“Hakuna manispaa isiyokuwa na hospitali, mashule, hivyo upo uwezekanao wa kukubaliana na hospitali hizo kununua dawa kutoka kwa wajasiriamali,” amesema na kuongeza.

“Pia ukiwaunganisha na shule na wanafunzi wote wa shule ya manispaa husika wakanunua sare za shule kutoka kwao, hii itawaongezea kipato na kutakuwa na maana ya kuwa na maeneo kama haya, ”ameshauri Chaurembo.

Naye Liana amesema ujenzi wa maeneo maalumu kwa ajili ya wajasiriamali utafanywa kwa wilaya zote tano.

Amesema kwa kuanza wameanza na Wilaya ya Kinondoni ambapo kituo cha Mwanyamala kinakamilika kabla ya kufanyika kwenye maeneo mengine.

“Wilaya nyingine tafuteni maeneo kwa ajili ya kujenga, hapa patakuwa na fremu za maduka kama mlivyoona, choo cha kulipia na kantini na fedha yote itakayopatikana itajazia mfuko wa kuwakopesha wanawake, vijana na walemavu, ”amesema Liana.

Liana amesema kuwa watahamisha baadhi ya vijana kutoka eneo la Mwenge wanakochonga vinyago na kuwapa nafasi katika eneo hilo.

Amefafanua lengo ni kulifanya liwe eneo la utalii na bidhaa mbalimbali, ili kusisimua biashara.

“Kuna vitu muhimu kama mlivyoona, maduka, vyoo, kantini, na maeneo ya biashara mbalimbali, tunataka kila kitu kipatikane kwenye eneo hili, ili mteja anapokuja asiondoke bila kununua bidhaa, ”amesema Liana.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz