Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wacharuka msimamizi mradi kukaidi maagizo

Madiwani Madiwaniiii.png Madiwani wacharuka msimamizi mradi kukaidi maagizo

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, wameonyesha masikitiko yao kwa baadhi ya wasimamizi wa miradi ya ujenzi kuwa pamoja na ushauri wanaotoa baada ya miezi mitatu wakikutana tena utekelezaji huwa hafifu.

Wakizungumza hayo jana Oktoba 26, 2023 kwenye kikao cha baraza la madiwani Kiteto baadhi ya madiwani hao wamesema pamoja na kushauri na kupendekeza kwa watumishi wa Serikali utekelezaji wake umekuwa hafifu.

Akizungumzia mradi wa jengo la mama na mtoto kata ya Makame, diwani wa kata hiyo Isaya Kinani ameonyesha masikitiko yake kuwa baada ya kushauri msimamizi wa mradi miezi mitatu iliyopita kwenye kikao cha baraza la madiwani kuwa fremu za milango ya jengo hilo zibadilishwe kwa kuwa ni fupi, mhandisi wa ujenzi huo na mafundi wake wao waliamua kuongeza vipande vya mbao juu na kufitisha milango kinyume na maagizo yao.

"Mwanzo Injinia tulimshauri kwamba fremu za milango ujenzi jengo la mama na mtoto kata ya Makame hazitatumika na zichongwe zingine upya na ndiyo yalikuwa maazimio ya baraza lililopita cha kushangaza zile zile fremu ambazo zilikuwa fupi ndizo zilizoongezewa vipande vya mbao juu. Sisi tulizikataa kwa kuwa zinaondoa uimara wa jengo letu...naomba sasa kupata ushauri zaidi na jibu lile kwa nini haya yanaendelea kutokea na tulishauri hapa miezi mitatu iliyopita?” amesema Isaya.

"Hizo fremu wamefitisha na plasta inaendelea kupigwa ukienda sasa unaweza kukuta jengo limekamilika kwa hiyo na mimi nashauri zoezi hilo la kuwasimamisha mafundi sasa lifanyike kwa haraka zaidi"amesisitiza Lendikushi kaimu afisa mipango wilaya

Kasimu Msonde ambaye ni Diwani Kata ya Kibaya, amesema lengo la Serikali katika miradi ni kuona inatumika kwa muda mrefu hivyo mradi kwa hali hiyo hauwezi kudumu na fedha zilizotolewa na Serikali haziwezi kuwanufaisha wananchi kikamilifu.

"Inafikia mahali mradi unaotegemewa na wananchi udumi kwa miaka hamsini za zaidi unadumu kwa miaka chini ya hapo na kuanza kukarabatiwa kitu ambacho kwa miradi ya maendeleo ya wananchi ni hasara sana," amesema Kasim Msonde.

Sakata la mipaka ya ndani ya wilaya na nje likaibuka tena ambapo hapa Diwani wa Kata ya Partimbo, Paulo Tunyoni anataka wakulima wa eneo lake wasisumbuliwe tena watakapoanza shughuli za kilimo.

"Kama wakulima wa eneo langu la utawala wako Kijiji cha Amei wafidiwe waondoke mle na kama hawako waendelee na kilimo chao na wasisumbuliwe tena ufikapo muda wa kilimo... sitaki watu wangu wasumbuliwe kiongozi mzuri ni yule anayelinda mipaka yake na wanaolinda mipaka ni pamoja na mimi kuanzia sasa naomba tusiingiliane kwenye mipaka,” amesema Tunyoni.

Kuhusu suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kiteto hapa anaonyesha msimamo wake na kisha mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kiteto anakiri changamoto hizo.

"Yaani hata kesho wee kimbia huko ukaone hali halisi ilivyo na kama utakuwa na usafiri ni vizuri na mhe ukamchukua mkaangalie hali ilivyo ukija huku uniambie hatua mliyochukua," amesema Mwenyekiti wa Halmashauri Bundala.

"Hili jambo la fremu mara ya kwanza zilikuja zikiwa haziendani na milango ikawa imeazimiwa kwenye kikao kama hiki cha madiwani zirudishwe zikafanyiwe marekebisho zimefanyiwa marekebisho na pia inaonekana hali sio sawa sawa," amesema mhandisi Antoni Lugiko kaimu mhandisi wa ujenzi halmashauri ya Kiteto.

"Nimelichukua tutalifanyia kazi hivyo nitakahikisha kuwa fremu hizo ambazo zimeungwa zinaondolewa mle kwenye ujenzi wa jengo la mama na mtoto kwa maelekezo hayo ya madiwani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live