Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani Mbozi wataka muda zaidi usajili laini za simu

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Baraza la madiwani halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe limeishauri Serikali ya Tanzania  kuongeza muda wa usajili wa laini za simu kutokana na wananchi wengi kutokuwa na vitambulisho vya Taifa vinavyotumika katika usajili huo.

Jambo hilo limeibuka leo Jumatano Julai 31, 2019 katika kikao cha baraza hilo baada ya madiwani hao kuhoji kuwa kasi ya utoaji wa vitambulisho hivyo haiendani na muda uliowekwa kwa ajili ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ambao umepangwa kufika kikomo Desemba 2019.

Diwani wa Wasa,  Ezekiel Mwashambwa amesema suala la vitambulisho vya Taifa limekuwa kero kwa wananchi hali iliyochangiwa na urasimu katika Idara ya vitambulisho vya Taifa.

"Zoezi la utoaji vitambulisho vya Taifa limechukua muda mrefu lakini bado idadi kubwa ya watu hawajapatiwa vitambulisho na wanaotakiwa kusajili laini zao wanapata usumbufu mkubwa ni vyea Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) kurejea vijijini kukamilisha uandikishaji,” amesema Mwashambwa.

Diwani wa Itumpi,  Richard Mahaya amesema Serikali ichukue hatua ya haraka kukamilisha usajili wa wananchi ili wapatiwe vitambulisho vya Taifa na kwamba katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Tanzania pekee ambayo raia wake hawana vitambulisho vya uraia.

Akijibu hoja hizo ofisa usajili wa Nida wilaya Mbozi, Rachel Fimbo amesema licha ya changamoto idara yake imefanikiwa kusajili watu 155,944 kati ya 251,697 sawa na asilimia 62.5.

Pia Soma

Ameeleza sababu inayokwamisha zoezi hilo ni pamoja na upotevu wa fomu.

Chanzo: mwananchi.co.tz