Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani Iringa wamgomea Hapi

34365 Pic+madiwani RC Iringa, Ally Hapi

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamegomea uamuzi wa mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi kuhusiana na ujenzi wa hospitali ya wilaya.

Katika kikao kilichoshirikisha wataalamu wa mkoa na halmashauri hiyo, baadhi ya madiwani na uongozi wa CCM, Hapi kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu aliagiza hospitali hiyo ijengwe Igodikafu badala ya kijiji cha Ihemi kilichopendekezwa na madiwani mwaka 2016.

Wakizungumza na wanahabari mjini Iringa jana, madiwani wanaopinga uamuzi huo walisema pamoja na maelekezo ya mkuu wa mkoa, hawakubali kuhamisha ujenzi wa hospitali hiyo kutoka kijiji cha Ihemi kwenda Igodikafu.

Diwani wa kata ya Masaka, Mathew Nganyagwa (CCM) alisema hakuna kamati yoyote wala baraza la madiwani lililowahi kukaa kubadilisha yaliyofanyika mwaka 2016 ya kujenga hospitali hiyo Ihemi.

Akikosoa uamuzi wa kujenga hospitali katika kijiji cha Igodikafu, Hapi alisema kijiji hicho kipo pembezoni mwa halmashauri hiyo kikiwa karibu zaidi na hifadhi ya Taifa ya Ruaha badala ya wananchi.

Naye diwani wa kata ya Luhota, Bruno Kindole (CCM) alisema uamuzi uliofanywa na mkuu wa mkoa si wa baraza kwa sababu halijawahi kukaa na kubatilisha kilichoamuliwa awali.

Naye, diwani kata ya Kiwele, Felix Waya (Chadema) alisema uamuzi wa kujenga hospitali hiyo Ihemi ulizingatia mapendekezo ya wataalamu na wakamuomba mkuu wa mkoa aagize liitwe baraza zima la madiwani ili mjadala ufanywe upya.

kizungumzia mamlaka aliyotumia kubadili uamuzi wa madiwani, Hapi alisema: “Tumefanya hivyo ili kusaidia mambo yaende, si kupora madaraka ya watu. Uamuzi wa mabadiliko haya ni wa pamoja, umeangalia maslahi mapana ya wananchi.”



Chanzo: mwananchi.co.tz