Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani Handeni wachagua mwenyekiti mpya wa baraza

40068 Pic+meya Madiwani Handeni wachagua mwenyekiti mpya wa baraza

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga, limemchagua diwani wa Kwamatuku (CCM), Mustaph Beleko kuwa mwenyekiti mpya wa baraza hilo. 

Uchaguzi wa mwenyekiti mpya umefanyika leo Jumatatu Februari 4, 2019 katika ukumbi wa halmashauri baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo Ramadhani Diliwa kujiuzulu nafasi hiyo Novemba mwaka 2018.

Jumla ya wapiga kura 22 wamepiga kura zote zilizompitisha diwani huyo kuwa mwenyekiti wao hadi mwaka 2020.

Awali msimamizi wa uchaguzi huo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni William Makufwe amesema imewabidi kufanya uchaguzi huo kwani ni miezi mitatu sasa nafasi hiyo ipo wazi.

"Mpaka sasa ni miezi mitatu hatuna mwenyekiti wa halmashauri, hivyo nimeandika barua kwa vyama vya CCM na Chadema kuomba wanipe majina ya madiwani ambao watapigiwa kura na nilipata jina moja la mgombea wa CCM ambaye ndio huyu atakayepigiwa kura," amesema Makufwe.

Mwenyekiti mpya Mustaph Beleko amewashukuru madiwani wenzake kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo na kuwaahidi kutoa ushirikiano kwao. 

"Nimepata uzoefu kutoka kwa mwenyekiti aliyestaafu (Ramadhani Diliwa) hivyo msiwe na wasiwasi nitaongoza kutokana na kanuni zetu zinavyosema," amesema Beleko.

Diliwa ajiuzulu kutokana na kipengele cha kwenye muktasari kinachosema uamuzi uliofanywa na baraza kuhusu makao makuu kuwa Kabuku haukuwa sahihi huku wajumbe wengine wa baraza hilo wakisema ni sahihi hatua iliyomfanya kujiuzulu. 



Chanzo: mwananchi.co.tz