Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madhara yatokanayo na tabia ya vijana kujichua

49656 Dk+Shita+Samwel

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kujichua kwa lugha ya kitaalam hujulikana kama masterbation. Ni tukio ambalo hufanywa zaidi na vijana kipindi wanapo balehe. Vijana na baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa wakijiuliza je, kuna madhara yatokanayo na huo mchezo?

Bado mijadala mbalimbali kuhusu hili tatizo limekuwa na migongano. Baadhi ya wataalamu na wanaharakati wao wanaona ni sawa tu kufanya hivyo kwani ni njia mojawapo ya kuepukana na maradhi.

Wengine wanasema ni burudani tu si vibaya kama mtu ataitumia kuridhisha nafsi yake. Leo nitadodosa kwa ufupi jambo hili angalau tupate picha kama ni salama au la.

Kitabibu au kisayansi kufanya tendo hilo kwa kiasi (mara moja kwa wiki) hakuna madhara, ila pale unapofanya kwa muda mrefu na kwa kutumia kasi ama nguvu sana inaweza kuwa na madhara ya kimwili na kiakili (kisaikolojia).

Wapo wanaofanya tendo hili kwa kutumia vilainishi kama sabuni, mafuta, losheni na huku wapo baadhi ambao hutumia mikono yao mikavu bila vilainishi.

Madhara ya kimwili ni pamoja na mchoko na ulegevu wa misuli, kupata michubuko au vidonda vinavyoleta maumivu, maumivu ya korodani, kuwa dhaifu kutokana na nguvu nyingi kupotea katika kufanya tendo hilo mara nyingi.

Madhara ya kiakili huwa ni makubwa zaidi ambayo yanaweza kuambatana na hali ya kukosa hisia kwa tendo asili yaani kujamiana na mwenza wa kike hii ni kutokana na mwili kuzoea kujiridhisha kwa njia hiyo.

Kuwahi kufika mshindo (premature ejaculation) na kutofika kileleni kutokana na mazingira ya usisimuliwaji kuwa tofauti na mazoea, kuchoka mapema na kukosa msisimko wa kupata hamu ya tendo la kawaida, hivyo kupungua kwa nguvu za kiume.

Tatizo hili linapomtawala mwanaume na akilifanya mara nyingi kwa siku huweza kumfanya kuwa na mwili usio na nguvu hii ni kwa sababu nguvu nyingi hutumika kwa ajili ya kitendo hicho.

Tatizo hili limekuwa likichangia mifarakano katika mahusiano ya wenza wawili hii ni kutokana na aidha kwa tatizo la kuwahi kufika mshindo au kutoridhika.

Ni vizuri kutoendekeza kujichua na ni vizuri kulifikiria jambo la kujamiana na mwenza utakayekuwa naye maisha kuliko kitendo hicho na kama ukishindwa basi usifanye kitendo hicho kupita kiasi na ufanye kwa kutumia vilainishi.

Vizuri wazazi kuzungumza na vijana wao bila kificho hasa wanapokaribia au wanapoonyesha dalili za kubalehe, ikumbukwe kipindi hiki ndiyo wengi hujiingiza katika tendo hilo.



Chanzo: mwananchi.co.tz