Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva watano wafungiwa leseni Arusha

Masejo Madereva watano wafungiwa leseni Arusha

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha katika kuhakikisha linakomesha matukio ya ajali kuelekea mwisho wa mwaka katika Mkoa huo limeendelea kutoa Elimu kwa madereva na kuwafungia leseni za udereva madereva watano (05) kwa makosa mbalimbali.

Akitoa taarifa hiyo leo Novermber 16 kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo asema kuwa madereva hao wamefungiwa leseni zao kwa muda wa miezi mitatu hadi sita kwa makosa mbalimbali ikiwemo ulevi, mwendokasi, kusababisha ajali, wenye makosa yanayojirudiarudia pamoja na wale ambao wanayapita magari mengine (overtaking) sehemu ambazo zimekatazwa kisheria.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kutoa elimu katika nyumba za ibada, stendi za mabasi, mashuleni, vijiwe vya bodaboda pamoja na masoko ambapo jamii hiyo imepata uelewa wa kutosha kuhusiana na sheria mbalimbali za usalama barabarani.

Aidha ACP Masejo ametoa onyo kali kwa madereva wanaoendele kuvunja sheria za usalama barabarani kuwa Jeshi hili halito muonea muhali dereva yeyote kwa makosa ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani.

Pia amewaomba wananchi kutoa taarifa za uhalifu na walifu ili kuuufanya Mkoa huo kuwa shwari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live