Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva waonywa kuendesha magari kwa mazoea

Madereva Waonywa Kuendesha Magari Kwa Mazoea Madereva waonywa kuendesha magari kwa mazoea

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madereva mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuendesha magari mabovu kimazoea ,kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao na kuleta madhara kwa watumiaji wengine wa barabara. - Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwayah, Mkuu wa operesheni kikosi cha usalama barabarani alipofanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto kilichopo Chimbuya mkoani Songwe. - “Dereva unatakiwa kujali usalama wako kwanza kisha kuwajali watumiaji wengine wa barabara ili kuweza kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika, ingiza gari barabarani likiwa zima na sio kuingiza gari bovu ambalo linakufanya usiwe na uhakika na safari uendayo mtambue kuwa sheria haijalala tunawachukulia hatua kwa makosa yote mliofanya ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii” amesema Kamanda Sisiwayah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live