Jeshi la polisi mkoa wa Tabora limewanyooshea kidole madereva wa mabasi ya shule na kuwataka kuwa msingi wa kutunza maadili ya nchi ikiwamo kuvaa kinadhifu na kuwa na muonekano mzuri kichwani wakati wakiwasafirisha wanafunzi.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Tabora Peter Magayane katika mkutano kati ya jeshi la polisi na wamiliki wa shule binafsi na mabasi uliokuwa unajadili mambo mbalimbali ikiwamo matukio ya ukatili dhidi ya watoto.
“Siyo unakuwa dereva umevaa hovyohovyo , umenyoa au una rasta,umevaa milegezo huwajengi wale watoto kuona kwamba wewe ni mtu mwenye tabia njema,” amesema Peter Magayane.