Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limewaonya madereva wanaoendesha Magari kutoka Bandarini kuelekea Nchi jirani maarufu IT kuachana na udereva wa kimazoea na badala yake kufuata sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Mrakibu wa Polisi (SP) Mosi Ndozero wakati akizumgumza na madereva hao katika Kituo Kikuu cha Polisi Mjini Iringa.
Ndozero amesema dereva atakayebainika kupakia abiria au kukutwa na nyaraka batili atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka kuzingatia sheria za Usalama barabarani.
Ameongeza kuwa, dereva hakatazwi kubeba mmiliki wa gari au kupakia mizigo isipokuwa anapaswa kuwa na Nyaraka zinazoonesha malipo ya mizigo husika na mhusika ambaye ni mmiliki wa chombo.
Amemaliza kwa kusema dereva atakaye kamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria.