Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva 17 wa IT wanaswa Pwani

Images (2 It.jpeg Madereva 17 mbaroni

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kibaha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia madereva 17 wa magari yanayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi (IT) kwa kosa la kusafirisha abiria kinyume cha sheria.

Magari hayo ya IT yanayoanzia safari zao Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi za Zambia, Rwanda, Burundi na Kongo kupita mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera inadaiwa yamekuwa yakisababisha ajali na kuleta madhara makubwa kwa abiria.

Kutokana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea na kusababisha vifo na majeruhi, jeshi la polisi mkoani humo limeanza operesheni ya kuwakamata madereva wote wa IT wanaokiuka sheria ya usalama barabarani.

Jana Alihamisi Desemba 29, 2022, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo amesema sheria ya usalama barabarani sura ya 168 inayokataza magari hayo kusafirisha abiria.

Lutumo ametoa wito kwa abiria kutumia usafiri rasmi wa umma ili kuepusha usumbufu wanaoweza kuupata safarini kwa kukosa haki zao za msingi inapotokea ajali watumiapo magari ya IT.

Amesema madereva wanaoendelea kukaidi na kuvunja sheria ya usalama barabarani kwa makusudi wataendelea kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Operesheni hiyo inafanyika ikiwa na kumbukumbu ya tukio la hivi karibuni la watu watano wakiwemo wanandoa Grayson Ngogo (50) na mkewe Janet Ruvanda (40) kufariki katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Morogoro.

Ajali hiyo ilitokea saa 6 usiku wa Desemba 25 mwaka huu baada ya gari ya IT Toyota Allion kugongana na lori la mafuta na kusababisha vifo vya watu hao watano wakiwemo wanandoa hao ambao walikuwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live