Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madarasa 21 yakamilika Kilimanjaro

Madarasa 21 Yakamilika Kilimanjaro.jpeg Madarasa 21 yakamilika Kilimanjaro

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro imekamilisha ujenzi wa miradi ya madarasa 21 , mabweni 12 pamoja na matundu ya vyoo katika shule nne za sekondari Kigonigoni, Nyerere (Lembeni),Vudoi na shule ya sekondari Msangeni.

Kukamilika kwa madarasa hayo pamoja ni mabweni kutasaidi kuboresha viwango wa ufaulu kwa wanafunzi na kuondoa adhaa ya wanafunzi kutembelea umbali mrefu.

Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amesema kukamilika kwa miradi hiyo itakwenda kutatua changamoto ya miundombinu mbinu katika shule hizo na kuleta chachu na kuongeza viwango vya ufaulu.

Tadayo amesema katika utekelezaji wa mradi wa kuongeza Enrollment ya wanafunzi wa Kidato cha Tano, Wilaya yetu ya Mwanga inatekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 21 na takriban mabweni 12 na matundu ya vyoo .

"Serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu imeleta fedha nyingi katika wilaya Mwanga na tayari miradi mingi ni kubwa imetekelezwa kwa asilimia kubwa,hivyo hatuna budi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali,"amesema Tadayo.

"Kwa ubunifu na matumizi mazuri ya fedha, wataalam wetu wameweza kuongeza vyumba vya ofisi za walimu katikati ya madarasa, Miradi yote hii ipo katika hatua mbalimbali za umaliziaji na kuhamia,"amesema.

Katika hatua nyingine, ahadi za CCM kupitia Mbunge wake Tadayo zinaendelea kutekelezwa ambapo zoezi la kukipandisha hadhi chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara ili kiweze kutoa shahada imekamilika na kwamba tayari udahili wanafunzi umeanza kwa ajili ya kuanza Mwaka wa kwanza wa Shahada mwezi Oktoba 2023.

Wakati huo huo, ujenzi wa chuo cha VETA Mwanga unaendelea kwa kasi katika eneo la Kisangiro ambapo awamu ya kwanza utakayohusisha majengo 9 inatazamiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi Nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live