Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madalali wadaiwa kuwadhalilisha kingono wafanyakazi wa ndani

Dada Wa Kazi Pic Madalali wadaiwa kuwadhalilisha kingono wafanyakazi wa ndani

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabinti wanaofanya kazi za ndani wameiomba serikali ipige marufuku madalali wanaotumika kuwezesha kupatikana kwao, wakidai wanashusha utu wa mwanamke.

Wamesema baadhi yao huwarubuni kwa rushwa ya ngono kwa ahadi ya kuwatafutia kazi nzuri, mshahara mnono na katika miji mikubwa, likiwamo Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Light for Domestic Workers, Beatrice Johnson aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT-T).

Alisema shirika hilo linalofanya shughuli zake mkoani Morogoro, limeshawafikia waajiri 72 na wafanyakazi wa ndani 250 kuwapa elimu kuepukana na ukatili wa kijinsia kama vile rushwa ya ngono na mimba.

"Hawa madalali wanaotumika kuwatafutia kazi mabinti, wamekuwa wakiwarubuni wasichana, utakuta wanakwenda maeneo tofauti mikoani kuwachukua wasichana na kuahidi kazi nzuri.

"Kutokana na wazazi kuahidiwa hayo, anamtoa mwanawe ili aje mjini kutafuta fedha kwa kufanya kazi za ndani. Madalali hawa walio wengi wanatambulika na mtu unawaamini, ila baadhi yao wanawaambia ukitembea naye anakupa kazi," alisema Beatrice.

Alisisitiza kuwa jamii inapaswa kufahamu kwamba Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya Mwaka 2004 inamlinda mfanyakazi wa nyumbani akiwamo mwenye umri wa miaka 14, ingawa changamoto ni wenye umri huo kufanya kazi zisizoendana na umri wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live