Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Watarajali Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro wadai kudhalilika mitaani kisa posho

DAKTARI MON Madaktari Watarajali Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro wadai kudhalilika mitaani kisa posho

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: JamiiForums

Mdau wa JamiiForums.com anadai Madaktari Watarajali (Interns) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa #Kilimanjaro (Hospitali ya Mawenzi) wapo katika wakati mgumu licha ya kujituma katika kutoa huduma Hospitalini hapo

Ametolea mfano kuwa malipo yao ya kila mwezi (Posho) ambayo yapo Kisheria, yamekuwa yakicheleweshwa ambapo posho ya Julai 2023 walilipwa Agosti 18, 2023 nayo ni baada ya kutishia kufanya mgomo, pia posho ya Agosti hadi kufikia Septemba 18, 2023 hawajalipwa na hawajapewa majibu watalipwa lini

Mdau anaomba Serikali iingilie changamoto hiyo kwa kuwa Madaktari hao Wanafunzi wanashindwa kulipa kodi katika makazi yao, pia anadai kuna uwezekano wa kuharibiwa Masomo yao ya Vitendo kwa sababu uamuzi wao wa kudai posho hauwafurahishi Viongozi wao.

=========

Sisi Watarajali (Interns) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Hospitali ya Mawenzi) tunapitia katika changamoto zenye kuleta ugumu mkubwa katika maisha yetu ya kulitumikia Taifa katika kutoa Huduma za Afya.

Tunapambana kwa juhudi kubwa katika kutoa Huduma za Afya hapa hospitalini licha ya kuwa na mazingira magumu ya utendaji kazi.

Tumekuwa tukipata shida sana kupatiwa stahiki zetu za Posho ya Interns ya kila mwezi, ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria, kumekuwa na desturi ya ucheleweshwaji mkubwa wa malipo ya posho zetu kila mwezi, ambapo huingiziwa posho zetu mwenzi wa mbeleni, tena tarehe zilizopitiliza.

Mfano posho ya mwezi wa Julai 2023, tulikuja tukaingiziwa tarehe 18 Agosti 2023 tena baada ya sisi wenyewe interns kuamua kukutana kujadiliana juu ya stahiki zetu, ndipo uongozi ulipata taarifa kuwa tunafanya kikao, wakaingiwa na hofu kwamba tunaweza kugoma, ndio wakaamua kulishughulikia na pesa tukaingiziwa jioni yake.

Hadi tarehe 17 Septemba 2023 posho yetu ya Agosti hatujapatiwa, tumefatilia kwa wahusika hakuna mwenye majibu yenye kueleweka kila mhusika anajibu “Mimi part yangu nimeshafanya”, hayo ni majibu tuliyoyazoea kila mwezi tukifatilia na huu ndio umekuwa utamaduni Hospitalini hapa kuchelewesha malipo ya Posho za Interns.

Hali hii imekuwa ikiiathiri sana maisha yetu kiasi ya kwamba hufikia miezi mingine watu hutolewa ndani ya vyumba vya watu kutokana na kushindwa kulipa kodi kwa wakati.

Kwa kweli tumekuwa wanyonge sana kwani wengi wetu, tumekuwa na hofu ya kufanyiwa figisu ya kuharibiwa Intership zetu endapo tukichukua hatu zitakao waudhi viongozi.

Tunadhalilika kwa kweli huku mtaani.

Chanzo: JamiiForums