Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madada poa 25 na wateja wao 5 mbaroni Dar

Changu 002 Madada poa 25 na wateja wao 5 mbaroni Dar

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko akiwa na Timuyake wiki hii wameendelea na oparesheni ya kushtukiza katika eneo la SinzaJijini Dar es salaam usiku wa kuamkia June 15,2024 kwa lengo la kuyabainina kuyafungia maeneo yanayotumiwa na Madada poa kuuza miili yao(Madanguro) ambapo wamefanikisha kukamatwa Watu 30 wakiwemo Madadapoa 25 pamoja na Wateja wao watano.

DC Bomboko amefanya msako wa lodge kwa lodge na gesti kwa gesti kwenyenyumba zote za wageni zilizokuwa zimebadilishwa kuwa Madanguro kwaMdada kulipa Tsh. elfu 10 kwa siku na kutumia chumba kujiuza siku nzima naWanaume tofauti ambapo ameagiza zifungwe huku akiwataka Wamilikiwajisalimishe ofisini kwake na ameagiza pia kufungwa kwa Bar na Night Clubkadhaa eneo la Sinza ambazo hutumiwa pia na Wadada hao kutafuta Watejawa kuwauzia miili yao.

DC Bomboko amesema; "Makaka poa na Madada poa, Mashoga na Wasagajiwote hawana nafasi katika Wilaya ya Ubungo na wote wanaofanya biasharahizi warudi wakafanye shughuli nyingine.

"Naagiza hawa wote waende kituo cha Polisi na baada ya Sikukuu wapelekwe Mahakamani na nielekeze oparesheniiwe endelevu maeneo yote, Watendaji wa Mitaa na Kata, Maafisa Tarafa naPolisi Kata na wengine Mimi nawaonesha mfano wajibu wa kupambana naMakahaba ni wa kwetu sote"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live