Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machinga toeni ushirikiano kuhamia eneo rasmi - RC Homera

Machinga Pc Databbb Machinga toeni ushirikiano kuhamia eneo rasmi

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewaomba wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga kutoa ushirikiano pale watakapotakiwa kuhamia maeneo rasmi yaliyotengwa kwa shughuli zao za kibiashara.

Mkoa huo ulikuwa bado haujatangaza maeneo rasmi ya machinga na kusababisha kufanyia shughuli zao maeneo tofauti ikiwamo sehemu za stendi ya magari.

Akizungumza leo Novemba 17 wakati wa mkutano wake na wamiliki wa viwanda na taasisi mbalimbali, Homera amesema machinga wanapaswa kutoa ushirikiano watakapotangaziwa kuhamia maeneo rasmi yaliyotengwa.

Amesema tayari wameandaa eneo la Airport ya zamani ambapo wameweka miundombinu safi na rafiki na kwamba hakutakuwa sababu za machinga yeyote kuleta mgogoro na kukataa kuhamia.

"Tayari barabara zinaendelea kuboreshwa na zinakuwa safi, umeme, maji, tumefunga taa za kisasa zaidi ya 100, lakini hata daladala, bajaji na pikipiki zote zitapaki pale, na zaidi kutakuwapo na uchomaji nyama yaani patachangamka, hivyo toeni ushirikiano" amesema Homera.

Amesema wakati machinga wakihamia huko Airport ya zamani, masoko ya Soweto, Block T na Sokomatola wafanyabiashara wataendelea na shughuli zao wakati wakiboresha miundombinu hadi itakapotangazwa vinginevyo.

"Sisi tunataka amani, marumbano hatutaki, hatuwezi kuwapeleka sehemu ambayo hatujaiandaa, wale wa Soweto, Block T na Sokomatola wataendelea na shughuli zao wakati tunakamilisha miundombinu" amesema Homera.

Chanzo: mwananchidigital