Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machinga mbaroni kwa wizi wa kichanga

Mtoto 1?fit=693%2C489&ssl=1 Machinga mbaroni kwa wizi wa kichanga

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la POLISI Mkoa wa Songwe linamshikilia Praxeda Msanganzila (28) Mkazi wa mtaa wa Ilolo, wilayani Mbozi kwa tuhuma za kuiba mtoto mdogo Mudrick Shula (siku 21).

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza nguo mtaani (machinga) alifanikisha wizi huo baada ya kumlaghai mama mzazi wa mtoto huyo Antifonia Mdolo (21) Mkazi wa mji mdogo wa Mlowo, Wilayani Mbozi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, Alex Mkama, alisema wizi huo ulitokea tarehe 12 Disemba mwaka huu, muda wa saa 12:00 jioni katika mtaa wa Tazara katika Mji mdogo wa Mlowo, Wilayani Mbozi.

Akieleza mazingira ya wizi huo, Kamanda Mkama alisema mtuhumiwa alimdanganya mama wa mtoto huyo baada ya kumuomba amsaidie kutafuta nyumba ya kupanga.

Alisema baada ya mtuhumiwa kufika nyumbani kwa mama mazazi wa kichanga huyo aliyeibwa alitengeneza urafiki wa muda mfupi hali iliyofanya mama wa mtoto huyo amuamini.

“Mtuhumiwa alifika nyumbani kwa mama wa mtoto (kichanga) na kuulizia vyumba vya kupanga na wakiwa wanaelekea kutafuta vyumba hivyo aliomba ambebe mtoto na baadae alitoweka katika mazingira ya kutatanisha” alifafanua Kamanda Mkama.

Alisema baada ya mtuhumiwa kutoweka na mtoto huyo mama wa mtoto alitoa taarifa polisi na kuanza msako wa kumtafuta mtoto huyo ambaye alipatika siku inayiofuata.

“Tumefanikiwa kumkata mtuhumiwa akiwa na mtoto huyo ndani ya nyumba yake baada ya majirani kutoa taarifa polisi kufuatia kelele za kulia kwa mtoto usiku kucha,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live