Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machinga Afrka Mashariki kushiriki maonesho Mwanza

917340834c9cc6cc1d1a48d8095aae97.jpeg Machinga Afrka Mashariki kushiriki maonesho Mwanza

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JUMUIYA ya wafanyabiashara wadogo zaidi ya 1,000 katika Ukanda wa Afrika Mashariki wanatarajia kufanya maonesho jijini Mwanza kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuuza bidhaa zao.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel alisema wajasiriamali wapatao 1,050 kutoka mataifa ya Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan na Burundi watashiriki maonesho na kuonesha shughuli zao katika viwanja vya Rock City Mall mwanzoni mwa mwezi ujao.

Gabriel alisema kuwa maonesho hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza yakiwa na lengo la kuchochea ukuaji wa sekta hiyo kiteknolojia na kuwahimiza kurasimisha shughuli zao wazifanyazo. “Hii fursa ya kipekee kwa vijana wa eneo hili lililonuia kujenga uchumi wa kijana kwa ajili ya kukuza ujuzi wao na kufanya uvumbuzi,” alisema Gabriel.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wadogo Afrika ya Mashariki (CMSEO-EA), Josephat Rweyemamu alisema maonesho hayo yaliyopewa jina maonesho ya Jua Kali/ Nguvu Kazi yana kauli mbiu isemayo “Kuhamasisha ubora na uvumbuzi ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara.”

Alitaja idadi ya wafanyabiashara wadogo na wa kati (katika mabano) watakaoshiriki kutoka katika kila nchi; Burundi (120), Kenya (381), Uganda (105), Rwanda (92), Sudan Kusini (53) na Tanzania wafanyabiashara 45. Rweyemamu alisema maonesho hayo yatawezesha kujifunza, kubadilishana ujuzi, kutengeneza mitandao wa wafanyabiashara na kujengeana uwezo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz