Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machifu, viongozi wa dini wakemea matukio ya ubakaji, ulawiti

Tue, 19 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya.  Viongozi wa dini na machifu wilaya ya Mbeya wamekemea vikali vitendo vya matukio ya ubakaji na ulawiti vilivyotokea  katika kitongoji cha Mageuzi Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi na kuitaka jamii kufichua watu wanaojihusisha na uovu huo.

Matukio hayo ambayo yameanza kuripotiwa tangu Februari 1, 2019 ambayo yanawakumba watoto walio na miaka mitatu hadi 12.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Machifu Wilaya ya Mbeya, Ezelina Mpoli akizungumza leo Jumatatu Februari 18, 2019 kwenye mkutano wa hadhara wa kujadili matukio hayo na namna ya kukabiliana nayo ili kulinda haki na usalama wa watoto.

Amesema matukio hayo yanasikitisha sana kwa namna moja hana nyingine yanahusishwa na imani za kishirikina.

"Sisi kama machifu hatutashindwa kukabiliana nayo  na tutahakikisha wahusika wanapatikana pia jamii toeni ushirikiano kwa vyombo vya Dora" anasema.

Diwani wa Nsalala, Kissman  Mwangomale amesema mpaka sasa watoto wanne wamebakwa na kwamba kabla ya kufanyiwa ukatili huo huvuliwa nguo .

"Licha ya watoto hao kubakwa jana (Jumapili) watoto watatu walinusurika baada ya mtu asiyejulikana aliwakuta wakichuma mapera jirani na kanisa la EAGT ambapo walikwenda kusali aliwachukua na kuwapeleka kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika kisha kuwalazimisha kuvua nguo jambo ambalo watoto walitekeleza," amesema.

"Baada ya kuvua nguo akawaeleza wachague adhabu ya kuchapwa viboko au kumwagiwa mchanga ndipo mmoja wa watoto ambaye  wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ushirika wa Mbalizi Vumilia   Mwasenga kukimbia  na kupiga mayowe ya kuomba msaada" anasema.

Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Mbalizi, Debora Lukololo amesema matukio hayo ni ya kusikitisha na kwamba hayavumiliki ni lazima wabakaji wapatikane popote walipo.

Anasema jamii inapaswa imwogope Mungu na kuachana na tabia ya kuamini imani za kishirikina katika kujipatia kipato.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT, Vumilia Mwasenga anasema matendo yanayotokea sasa nchini hayampendezi Mungu na hivyo Watanzania kwa imani za dini zetu tunapaswa kufunga na kuomba.



Chanzo: mwananchi.co.tz