Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabinti wapewa baiskeli kukwepa vishawishi vya kingono

Mabinti Mskl Mabinti wapewa baiskeli kukwepa vishawishi vya kingono

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Plan International limetoa jumla ya baiskeli 500 kwa wanafunzi wa kike wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwaondolea adha ya usafiri waendapo shule na kuwapunguzia hatari ya vitendo vya ukatili wa kingono.

Msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwezesha Mabinti Balehe Kuendelea na Masomo (KAGIS) unaosimamiwa na shirika hilo katika mikoa ya Geita na Kigoma chini ya ufadhili wa Watu wa Canada (CAG).

Akizungumuza wakati wa hafla ya utoaji baiskeli hizo mjini Geita, Mkurugenzi wa Miradi Plan International Tanzania, Peter Mwakabwale amesema baiskeli 300 zimetolewa kwa wasichana wa mkoa wa Geita na 200 mkoani Kigoma.

Amebianisha hiyo ni awamu ya kwanza ya mpango huo na hadi kukamilika kwa mradi wa KAGIS wamepanga kununua na kugawa jumla ya baiskeli 2,000 kusaidia kufikiwa adhima ya upatikanaji sawa wa elimu msingi kwa makundi yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live