Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabehewa ya treni yaacha njia Kigoma

Behewaa Weeb Mabehewa ya treni yaacha njia Kigoma

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: eatv

Abiria zaidi ya 500 waliokuwa wakisafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea Jijini Dar es Salaam na mikoa mingine kwa njia ya reli wamenusulika kupata ajali, baada ya behewa tatu kuacha njia na kusababisha taharuki kubwa.

Ajali hiyo imetokea eneo la Kibirizi, muda mchache tu baada ya kuanza safari, ambapo baadhi ya mashuhuda ambao pia ni abiria waliokuwa wakisafiri, wameeleza hali ilivyokuwa huku wakiomba kufanyika ukaguzi kabla ya kuanza safari.

Msaidizi wa Steshebni Masta Shirika la Reli Nchini TRC mkoa wa Kigoma Evarsti Mshana, amesema hadi sasa hakuna athari zozote zilizotokea, na wanaendela na uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo.

Chanzo: eatv