Idadi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya barabarani iliyotokea leo majira alfajiri mkoani Mwanza, imeongezeka na kufikia watu nane.
Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la abiria mali ya kampuni ya Nyehunge lililogongana na basi la Asante Rabi katika eneo la Ukiriguru Wilaya ya Misungwi, watu wengine 39 wamejeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T458 DYD lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea Jijini Arusha kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari na hivyo kuligonga basi la Nyehunge lililokuwa linatokea Morogoro kwenda mkoani Mwanza.