Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabaharia wazoa takataka mto Mirongo kulinda Ziwa Victoria

IMG 4384.jpeg Mabaharia wazoa takataka mto Mirongo kulinda Ziwa Victoria

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Mabaharia na wadau wengine wa usafirishaji kwa njia ya maji wanaoshiriki maadhimisho ya Kiaifa ya siku ya Mabaharia duniani jijini Mwanza wameshiriki kampeni ya uhifadhi wa mazingira kwa kuondoa taka ngumu ndani yam to Mirongo inayomwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria.

Akizunguza na waandishi wa habari leo Juni 23, 2023, Kaimu Meneja Mafunzo na Utoaji vyeti kwa Mabaharia kutoka Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC), Lameck Sondo amesema wameamua kufanya usafi kwa kuondoa taka ngumu ndani yam to Mirongo kulinda mazingira, mazalia na usalama wa vyombo vya usafirishaji ndani ya Ziwa Victoria.

‘’Maji ya mto Mirongo yanaenda moja kwa moja ndani ya Ziwa Victoria, tumeamua kufanya usafi kuzuia taka ngumu kuingia ziwani kuathiri mazalia ya samaki na viumbe hai wengine majini,’’ amesema Sondo

Nahodha wa meli kutoka kampuni ya Mkombozi, Magoko Marwa amesema licha ya kuathiri viumbe hai, taka ngumu zinazoingia ndani ya ziwa pia uhatarisha usalama wa vyombo na abiria kwa kunasa kwenye pangaboi na hivyo kuathiri utendaji wa injini wakati wa safari.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Mande Mangapi, nahodha wa meli kutoka kampuni ya Kamanga Ferry akisema; ‘’Uchafu unaotokana na taka ngumu huathiri mfumo wa kupooza mitambo kwenye vyombo vya usafirishaji majini. Tunaiomba Serikali kupitia mamlaka husika ziwabane wote wanaotupa takataka ndani ya mito inayomwaga maji Ziwa Victoria,’’

Baharia Najma George kutoka Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) amewaasa wakazi wa wilaya za Ilemela, Nyamagana, Magu na Misungwi anakopita mto Mirongo kabla ya kumwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria kuacha tabia ya kutupa takataka ndani yam to huo ili kulinda siyo tu mazingira, bali pia viumbe hai majini.

‘’Takataka ngumu zinapoingia ziwani hujikusanya na kuingia kwenye propela za meli na hivyo kuhatarisha usalama wa vyombo vya majini, abiria na mali zao,’’ amesema Najma Siku ya mabaharia duniani huadhimishwa Juni 25 kila mwaka ambapo kitaifa yanafanyika jijini Mwanza yakiambatana na maonyesho ya vifaa na huduma mbalimbali zinazohusiana na usafirishaji majini.

Chanzo: Mwananchi