Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini

35187 Pic+maandamano Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini

Tue, 8 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kurejesha kikokotoo cha mafao cha zamani yakisubiri kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, huduma zimesimama kwa baadhi ya taasisi.

Wafanyakazi wameandamana leo Januari 07, 2019 kutoka eneo la Bunge hadi Uwanja wa Nyerere Square na sasa wanamsubiri Waziri Mkuu kuwapokea.

Mwananchi ilifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kukuta shughuli za wodini na mapokezi zikiendelea lakini baadhi watendaji hawakuwepo.

Katika ofisi ya mganga mfawidhi wa mkoa hakukuwa na huduma ambapo foleni ilikuwa ndefu mlangoni lakini ikaelezwa kuwa wapo kwenye maandamano.

Ofisi za Jiji (Elimu) hakukuwa na watumishi na watu waliokwenda kwa huduma ikiwemo wazazi wenye wanafunzi waliokuwa na mahitaji wameweka foleni ndefu bila huduma.

"Wamesema viongozi wako kwenye maandamano,  hatujui muda gani tutapata huduma na tunatoka mbali," amesema Job Muhumpa.

Mzazi huyo amesema maandamano hayo yangefanyika siku ambayo si ya kazi wasingeathirika kwa kiasi hicho lakini haina maana kufanya siku za kazi tena siku ambayo watoto wanatakiwa kuripoti shuleni.



Chanzo: mwananchi.co.tz