Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandalizi ya kuwahamisha kwa hiari wamasai wa Ngorongoro yakamilika

Masai Mkao Maandalizi ya kuwahamisha kwa hiari wamasai wa Ngorongoro yakamilika

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya imesema wakati wowote kuanzia sasa familia 100 za jamii ya kimasai zitawasili katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya kuwahimisha kutoka yaliyokuwa makazi yao yaliyopo katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana alipotembelea kijiji hicho kwa lengo la kufanya tathmini ya maandalizi ya kuwapokea wageni hao.

“Tumekuja kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa makazi, na huduma za kijamii kwa wananchi watakaohamia hapa. Nimeridhika sehemu kubwa ya miundombinu imekamilika, muda wowote kuanzia sasa wanangorongoro waliojiandikisha kwa hiari watahamia hapa kuendelea na maisha ili kupisha shughuli za Uhifadhi ndani ya eneo,” amesema Waziri Chana.

Pia ameendelea kusema kuwa, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 103 na huduma zingine za kijamii,

Serikali inajipanga kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za makazi 400 kwa ajili ya kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhamia Msomera.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ingawa amekiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto ikiwemo kasi ndogo katika uboreshwaji wa baadhi ya miundombinu kama vile umeme, mawasiliano pamoja na barabara, lakini amesema yote yanafanyiwa kazi.

Ingawa hatua ya kuwahamisha wananchi wa jamii ya Kimasai kutoka Ngorongoro imekuwa ikikosolewa na baadhi ya wanaharati, serikali imekuwa ikisisitiza kwamba wananchi hao wanaondoka kwa hiari ili kupisha shughuli za uhifadhi kufanyika katika eneo hilo ambalo liko katika orodha ya urithi wa dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live