Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maambukizi ya VVU yapungua Lindi

Ummy 7c676d638 Maambukizi ya VVU yapungua Lindi

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Mkoa wa Lindi kutoka asilimia 2 hadi asilimia 1.7 mwama 2023 ambayo imepelekea kufikia malengo ya 95-95-95 katika Mkoa huo huku Viongozi wa Mkoa huo wakitakiwa kutobweta bali waendelee kuchukua hatua kwa kutoa elimu.

Wazir Ummy amesema hayo akiwa katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Lindi baada ya kutembelea katika Kituo cha Afya Mnazimmoja, Kituo cha Afya cha Mjini, Zahanati ya Nachingwea pamoja na kutembelea Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi.

“Niwapongeze Mkoa wa Lindi mmefikia malengo ya 95-95-95 ambapo asilimia 96 ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanajua kwamba wana maambukizi ya UKIMWI, asilimia 95 ya Watu wenye maambukizi wapo kwenye dawa na katika asilimia hiyo 95 ya wanaotumia dawa virusi vimefubazwa”

Waziri Ummy amewataka Wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi, ulaji wa vyakula kwa kupungua chumvi nyingi, sukari nyingi na mafuta mengi ili kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari “Miaka Mitano iliyopita huwezi kuona Kisukari, huwezi kuona shinikizo la juu la damu kwenye magonjwa matano yanayowasumbua Watanzania wengi”

Waziri Ummy anatarajia kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi leo Machi 1, 2024 baada ya kutembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (Sokoine) pamoja na kuzungumza na Kamati ya Afya Ngazi ya Mkoa (RHMT)na Kamati ya Afya Ngazi ya Wilaya (CHMT).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live