Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu! mtoto aliyefariki 2017 adaiwa kufufuka Geita-VIDEO

Afufuka Geita Maajabu! mtoto aliyefariki 2017 adaiwa kufufuka Geita

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linaendelea na uchunguzi wa tukio la mtoto aitwaye Leonard Morisha (11) aliyefariki dunia Juni 27 mwaka 2017 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa ugonjwa wa kuishiwa damu, ambapo ameonekana hai, huku wazazi wake wakimtambua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamshina Msaidi Henry Mwaibambe amesema Mtoto huyo aliyekuwa anaishi na wazazi wake, alizikwa nyumbani kwao Kijiji cha Ngemo Wilaya ya Mbogwe ambapo alipatikana Oktoba 2021 akiwa hai huko katika kijiji cha Segese Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga .

Kamanda Mwaibambe amesema Disemba 12. 2021 baadhi ya wenyeji wa kijiji cha Ngemo wakiwa wanafanya vibarua maeneo ya Segese walimuona mtoto huyo na kumkumbuka ambapo walichukua jukumu la kuwapigia simu ndugu zake.

View this post on Instagram

A post shared by Clouds TV ???????? (@cloudstv)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live