Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya Dk. Mpango kwa wasimamizi Mto Rufiji

Mpango Pc Data Rfii Philip Mpango, Makamu wa Rais

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Makamu wa Rais, Dk Phillip Mpango amewataka Wakuu wa Wilaya na Mikoa inayozunguka bonde la Rufiji ambayo maji yake yanamwaga kwenye mto Rufiji kusimamia uhifadhi wa Mazingira.

Dk Mpango amesema hayo alipotembelea bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kusafiri kwa treni ya Tazara na kupokelewa katika stesheni ya Fuga na kupata fursa ya kujionea kazi za mradi huo zikiendelea.

Amesema kwamba katika suala la usimamizi wa mazingira atakuwa mkali na mstari wa mbele kufatilia na watakaozembea atatumia rungu lake kama msimaizi mkuu.

Aidha amewatataka wanasiasa wakiwemo wabunge kushiriki katia kutoa elimu kupitia mikutano yao na wananchi juu ya umuhimu na faida za utunzaji wa mazingira, kwani bwawa la Nyerere linategemea kupata maji kutoa kwenye vyanzo mbalimbali na bila kufanya hivyo serikali itarudi nyuma.

Aidha, Dk Mpango amewataka wasimamizi wa Mradi huo kitengo cha ushauri wa uhandisi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) (TECU)kuzingatia ubora na viwango vya kitaalamu.

Msimamizi wa Mradi toka kitengo cha ushauri wa uhandisi wa Wakala wa Barabara nchini -Tanroads (TECU), Mhandisi Mkazi John Mageni, amesema pindi mradi huo utakapokamilika, maji ya kulijaza bwawa kikamilifu litachukua miezi miname hadi lijae.

Mageni pia amesema mpaka sasa mkandarasi wa mradi huo amekwishalipwa zaidi ya Sh2.8 tirioni.

Chanzo: mwananchidigital