Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ma-RC wakutana kujadili mambo manne, wapewa agizo

Ma Rcp Ic Data Ma-RC wakutana kujadili mambo manne, wapewa agizo

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wakuu wa mikoa sita ya Nyanda za Juu Kusini wamekutaka kujadili hali ya usalama wa chakula, mipaka, uvamizi wa hifadhi na usafirishaji huku Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ikiwaagiza kuangalia namna ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa nchi jirani.

Wakuu hao wa mikoa waliokutana leo Jumatano Januari 26, 2022 ni pamoja na wa Mkoa wa Mbeya, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Songwe, Iringa na Njombe. 

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera amesema kikao hicho ambacho pia kilihusisha kamati za ulinzi la usalama za mikoa kimejadili masuala menne ikiwamo hali ya usalama wa chakula, usalama wa nchi kupitia maeneo ya mipakani na usafirishaji wa bidhaa kupitia uwekezaji wa njia za miundombinu ya barabara, bandari na reli zilizopo katika mikoa hiyo pamoja na uvamizi wa hifadhi.

Homera ambaye ni mwenyeji katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mbeya amesema ''Tunazo ajenda nne ni kujadili hali ya chakula na mahitaji kama tunavyoona mvua zimechelewa kunyesha na hivyo kusababisha ukame katika maeneo mengi nchini na kuweka mikakati ya pamoja  ya  kutoka na maadhimio ambayo tutayafanyia kazi'' amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Exsaud Kigahe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho, amesema kuwa kupitia kikao hicho ameagiza wakuu wa mikoa kuona namna ya kuondoa vikwazo vya kiuchumi kupitia nchi jirani jambo linalosababisha kuwepo kwa changamoto za kufungiana mipaka.

Amesema kuwa ufike wakati sasa kufungua fursa za kiuchumi  kwa kuondoa vikwazo kwa nchi jirani kwa kuzingatia kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni lango la kiuchumi kwa  kuingiza bidhaa kupitia mipaka ya Tanzania na nchi jirani za Zambia na Malawi .

''Wakuu wa mikoa tengenezeni mazingira wezeshi ya kuondoa vikwazo vya kibiashara wakati Serikali ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara, reli na bandari hivyo ni jukumu lenu kuona vikwazo hivyo vinaondoka'', amesema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz