Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ma RC wachuana kutangaza fursa za uwekezaji

88495 Uwekezaji+pic Ma RC wachuana kutangaza fursa za uwekezaji

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Wakuu wa Mikoa ya Tabora, Geita na Kigoma juzi walitumia kongamano maalum lililoandaliwa na Benki ya CRDB kushindana kutangaza fursa za biashara na uwekezaji katika mikoa yao.

Kongamano hilo la uwekezaji lililofanyika mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wafanyabiashara, makandarasi na wazabuni liliongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robart Gabriel alianza kwa kusifia Mkoa wake kuwa eneo sahihi la uwekezaji kutokana na uwepo wa fursa na rasilimali kadhaa ikiwemo ardhi, maliasili na madini.

Huku akimrushia kijembe mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, mkuu huyo wa mkoa wa Geita amesema, “huwezi kuulinganisha na mkoa wa Geita na mkoa wa Tabora unaotegemea zao la tumbaku na pamba inayolimwa kwa kutegemea mvua, sisi tunavuna dhahabu kila siku,”

“Mwaka huu katika kipindi cha miezi 10 tumepata kilo 2,522 za dhahabu yenye thamani ya Sh237 bilioni na Serikali imepata tozo ya Sh18.8 bilioni.”

Mwanri amesema Mkoa wa Tabora ndio unaotegemewa na Taifa kwa uzalishaji wa pamba mbegu na kutamba kuwa licha ya kupewa makadirio ya kuzalisha tani 850,  wamezalisha zaidi ya tani 15, 000 za pamba mbegu.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga naye hakubaki nyuma amesema Mkoa wake umejaliwa eneo kubwa la ardhi, nzuri na yenye rutuba inayofaa na kustawisha mazao yote ndiyo maana haijawahi kuwa na historia ya upungufu wa chakula licha ya kupokea na kuhudumia watu kutoka mikoa yote nchini pamoja na wakimbizi kutoka nchi jirani.

Baada ya kusikiliza wakuu hao wa mikoa wakitambiana, Bashungwa amewapongeza kwa uwezo wao wa kutangaza fursa na kuvutia wawekezaji katika maeneo yao na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizotajwa na viongozi hao.

Ofisa biashara mkuu wa CRDB, Joseph Witts amesema benki hiyo yenye amana za zaidi ya Sh5 trilioni  rasilimali zenye thamani ya Sh7 trilioni  imetenga zaidi ya Sh3.4 trilioni kwa ajili ya mikopo kwa wafanyabiashara, makandarasi na wazabuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz