Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSD yapewa eneo ujenzi wa Ghala

Msd Ghala MSD yapewa eneo ujenzi wa Ghala

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella, ameuhakikishia uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuwakabidhi eneo la ujenzi wa Ghala la kuhifadhia Bidhaa za Dawa kwa mkoa huo kabla ya mwezi Januari 2024 ili kurahisisha usambazaji wa dawa mkoani humo.

Mongella amesema hayo katika kikao kazi cha Bohari ya Dawa (MSD) na wateja wake kanda ya Kilimanjaro kilichofanyika mkoani Arusha na kuipongeza MSD kwa kusambaza bidhaa za Dawa nchi nzima pamoja na uwepo wa changamoto za miundombinu kwa baadhi ya maeneo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai amesema Bohari ya Dawa imedhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa bidhaa za Dawa kutoka nje ikiwemo kuongeza uzalishaji nchini hali itakayopunguza uagizaji huo wa bidhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live