Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MM yatwaa ubingwa wa Ryder Cup 19 Arusha

64967 PIC+GOLFU

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Timu ya Golf ya MM imefanikiwa kutwaa ubingwa na michuano ya Ryder Cup 2019 kwa kupata jumla ya pointi 14.5 dhidi ya timu ya Break Fast Lugalo iliyopata pointi 6.5.

Katika michezo hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya Mwananchi Communication, jumla ya wachezaji 28 walishiriki kutoka mataifa ya Zimbabwe, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania.

Katika michezo mitano ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa kiliGolf timu ya MM ilishinda pointi 4-1 za Break Fast na michezo sita ya pili MM ilishinda pointi 4-2 katika uwanja wa Gymkhana.

Akitangaza matokeo ya fainali jana michezo 10 ilichezwa  uwanja wa KiliGolf, Nahodha wa Ryber Cup 2019 kutoka klabu ya Break Fast alisema MM imepata  pointi 6.5 dhidi ya break Fast iliyopata pointi 3.5.

"Mwaka 2017 Break Fast ilitwaa kombe na mwaka huu MM imeshinda," alisema.

Nahodha wa Timu ya MM, Stephen Lukanyo akizungumza baada ya kukabidhiwa kikombe alisema mashindano mwaka huu yalikuwa magumu na wanashukuru wachezaji wenzake kwa ushindi.

Pia Soma

Alisema michuano hiyo mwakani itafanyika nchini Uganda.

Wadhamini wengine mbali na Mwananchi walikuwa ni Strategic Insurance, Woolworths na Gard world.

Chanzo: mwananchi.co.tz